Menu
 

Jumuiya ya vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Wilaya ya Mbeya Vijijini wanatarajia kuwaazimia viongozi wa chama hicho na viongozi wa Serikali kung;'olewa katika nafasi zao kutokana na kile kilichoelezwa kuwa hawajaweza kushirikiana na wananchi kutatua kero zao za maendeleoeo.

Habari kutoka ndani ya UVCCM zimelieleza mtandao huu kuwa maazimio hayo yatafikiwa katika kikao cha Baraza kuu la vijana wa wilaya hiyo kinachotarajia kufanyika Agosti 30 mwaka huu wilayani humo baada ya kufunguliwa na viongozi wa chama hicho.

Chanzo chetu cha kuaminika kutoka ndani ya Baraza hilo ambalo ndiyo mahala pekee pa vijana hao kuzungumzia kero zao juu ya chama na Serikali kimesema kuwa mbali na maazimio yatakayowalenga moja kwa moja viongozi wote wa Chama na Serikali kutoka ngazi ya shina mpaka Taifa, pia suala la kujivua gamba litazungumzwa kwa upana na marefu na kulitolea maazimio.

''Unajua viongozi wengi wakipewa madaraka wanajisahau badala ya kuwatumikia wananchi wanatumikia ofisi zao na familia hivyo baraza hilo litakuwa moto sana, lenmgo ni kuwarejeshea imani vijana ambao wanadhani kuwa ndani ya CCM ni sawa na dhambi na zaidi waandishi wa habari wataitwa ili kuweka wazi maazimio ya baraza hilo'' kilisema chanzo hicho ambacho kiliomba hifadhi ya jina na wadhifa.

Habari za uchunguzi zimebaini kuwa kati ya viongozi wanaotarajiwa kutolewa maazimio na vijana hao ni pamoja na Katibu wa CCM wa wilaya hiyo Nicolaus Kasendamila kwa kile kilichoelezwa kuwa kutokuwa na mahusiano mema na vijana hao na hasa kipindi cha uchaguzi Mkuu uliopita 2010 ambao vijana na baadhi ya wagombea wa nafasi ya udiwani walimtupia lawama.

Baraza hilo linalotarajia kuhusisha wajumbe kutoka kata 25 zilizopo ndani ya wilaya hiyo linatoa nafasi ya kila mjumbe kutoa dukuduku lake ndani ya kikao hicho ikiwa ni pamoja na kuzungumzia mwenendo wa Serikali na viongozi wake kuanzia Serikali za vijiji mpaka Taifa.

Katibu wa UVCCM wa wilaya hiyo Frank Kibiki ambaye alithibitisha kuwepo kwa kikao hicho Jumanne ya Agosti 30 mwaka huu ambaye alisema kikao hicho kipo kikatiba na baraza hilo linatakiwa kuketi mara mbili kwa mwaka lakini alisema hawezi kuzungumzia maazimio yanayoweza kutolewa na baraza lake.

Sanjari na hayo kutokana na hali ya mwenendo ulivyo hivi sasa katika Serikali na ndani ya chama hicho vijana wengi wa UVCCM wamenyongea na kukosa matumaini huku wakizungumzia zaidi suala la kujivua gamba ambalo wanadai kuwa linalenga kunyosheana vidole badala ya uhalisia ulivyo ndani ya chama hicho kwa ujumla wake.chama hicho. 

Wakati huo huo, leo hii Chama Cha Mapinduzi (CCM) kinatarajia kufanya mkutano wa hadhara katika mji mdogo wa Tunduma ambako ni ngome kuu ya Chadema katika Mkoa wa Mbeya.

Taarifa za uhakika kutoka ndani ya chama hicho zimeuleza mtanda huu wa www.kalulunga.blogspot.com zimetanabaisha kuwa kikosi hicho kitaongozwa na Samwee Shitambala.

Vijana waliozungumza mtandao huu ambao wengi wao ni viongozi wa Jumuiya ya UVCCM wamesema kuwa kutokana na mparaganyiko ulivyo ndani ya chama hicho imefikia hatua hata wajumbe wa vikao vya jumuiya mbalimbali wameshindwa kuhudhuria vikao vinavyowahusu kutokana na vikao vingi kuwa na mwelekeo wa kukomoana badala ya kuhimarisha

Post a Comment

 
Top