Menu
 

                 Hapa ni Stendi ya Uyole jijini Mbeya
Baadhi ya vijana waishio kata za Uyole, Itezi, Igawilo na Gombe wamebuni njia mpya ya utapeli wa fedha kwa kutumia picha za baadhi ya watu wanadaiwa kuwa wamekwisha fariki dunia.

Baadhi ya wananchi waliokutwa eneo la Stendi ya Uyole wamesema kuwa wamekuwa wakilazika kuchangia fedha kama rambi rambi kwa baadhi ya vijana ambao wamapita kuchangisha mchango kwa madai kuwa wamefiwa ndugu zao.

Kutokana na kuibuka kwa vitendo hivyo wakazi wa eneo hilo wameuomba uongozi wa Serikali za mitaa kutumia vijana waaminifu kuchangisha michango ili kuondoa hatari kwa wananchi kuvunjika mioyo ya utoaji kutokana na hofu ya kutapeliwa.

Post a Comment

 
Top