Menu
 

Huu ni Mtandao wa Watangazaji na Waandishi wa habari wa Redio Mkoani Mbeya.

Vyombo vya habari mkoani Mbeya vimeombwa kutoa msaada wa kutangaza kazi za wasanii chipukizi badala ya kutangaza zaidi kazi za wasanii maarufu hapa nchini.

Ombi hilo limetolewa na mmoja kati ya watayarishaji wa kazi za mziki wa kizazi kipya mkoani hapa kutoka studio ya Lizy Records Bwana Daniel Shirima wakati wa mahojiano na Bomba Fm 104.0MHz kuhusu namna ambavyo anasaidia vijana wenye vipaji vya uimbaji ili kujikwamua kimaisha.

Amesema mkoa wa Mbeya una wasanii wengi wazuri lakini wamekuwa wakishindwa kupata msaada wa kuendelea na kutangaza kazi zao kutokana na idadi kubwa ya wafanyakazi wa vyombo vya Redio jijini hapa kutangaza zaidi kazi wasanii maarufu.

Hata hivyo amewataka wasanii kuondokana na tabia hatarishi ili waweze kufikia malengo ya kazi zao za sanaa. 

Post a Comment

Anonymous said... 22 August 2011 at 09:37

safi sana kwa moyo huo kwani Wanahabari ni moyo wa wananchi na Mungu awajalie MBN msimame

UKURASA MPYA HUU said... 22 August 2011 at 13:27

Okay nashukuru sana ndugu yangu kwa changamoto yako kaka, natambua umuhimu wako na endelea kutembelea mtandao huu.

 
Top