Menu
 

Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Bwana JOHN LIVINGSTONE MWAKIPESILE

Taarifa zilizotufikia mtandao huu zimeeleza kuwa waandishi wa habari wa mkoa wa Mbeya waliofika katika ofisi ya Mkuu wa mkoa wa Mbeya kwa ajili ya kuzungumza nae kwa mwaliko wa ofisi yake wamesusia kikao hicho baada ya kuachwa solemba nje ya ofisi zaidi ya masaa mawili.

 Waandishi hao wamesema kuwa mwaliko huo ulionesha kuwa mazungumzo kati yao na Mkuu huyo wa mkoa wa Mbeya yalitakiwa kuanza saa 8 kamili mchana lakini wamekaa nje ya ofisi hiyo tangu muda huo mpaka saa 9.25 alasiri.

 Wamesema kuwa baada ya kuona hivyo wameamua kuondoka eneo hilo na kuendelea na shughuli zingine ambapo wamesema mhariri mkuu wa mtandao huu alifanya vema kukataa kwenda baada ya kupata taarifa za mwaliko huo kupitia wanahabari wengine wakati wanaelekea ofisi hizo za Serikali.

Post a Comment

 
Top