Menu
 


Wafanyakazi wa halmashauri ya jiji la Mbeya kitengo cha usafi ndani ya jiji wanakabiliwa na hali ngumu ya utendaji kazi kutokana na uhaba wa vitendea kazi.Wakiongea na mtandao huu wafanyakazi kumi ambao walikutwa wakifanya kazi zao katika mazingira magumu wamesema kuwa uhaba wa vitendea kazi katika shughuli zao unachangiwa kwa kiasi kikubwa na halmashauri ya jiji kushindwa kufanya kazi kwa usahihi.Kitengo hicho kinajihusisha na usafi wa barabara, sehemu za biashara na maeneo ya wazi ya jiji la Mbeya ambapo Bomba Fm imekuwa wafanyakazi hao wakitumia fagio na koleo wakati huohuo hawana vitu vitakavyowasaidia kujikinga dhidi ya magonjwa ya mripuko.Naye Mkurugenzi wa jiji la Mbeya Bwana Jummanne Idd amekiri kupokea malalamiko hayo na kusema kuwa vifaa vya kufanyia usafi vipo lakini baadhi yao wamekuwa hawavitunzi vizuri.

Post a Comment

 
Top