Menu
 

Wakazi wa mji mdogo wa Mbalizi wilaya ya Mbeya vijijini mtaa wa Tarafani wako hatarini kukumbwa na magonjwa ya milipuko kutokana na vyoo vya soko kujaa na kutiririsha maji kwenye makazi ya watu na maeneo ya biashara.

Wakazi na wafanyabiashara hao wameuomba uongozi wa halmashauri ya wilaya ya Mbeya kuchukua hatua za haraka kunyonya majitaka hayo kwenye vyoo ili kuwanusuru dhidi ya magonjwa hatarishi kama kipindipindu.

Bi.Neema Sanga ambaye ni mfanyabishara wa eneo hilo amesema zimepita siku tatu tangu vyoo hivyo vianze kutiririsha maji taka mitaani lakini hakuna hatua zozote zinazochukuliwa ili kuwanusuru katika hatari ya kupatwa na magonjwa ya miripuko.

Naye mwenyekiti wa soko hilo BI.Grace Nyato amesema taarifa za kujaa kwa vyoo hivyo zimekwishatolewa ofisi ya mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ili waweze kulipatia ufumbuzi tatizo hilo.

Post a Comment

 
Top