Menu
 

 Kamanda wa Polisi Mkoani Mbeya Advocate Nyombi.
Wakazi wa maeneo ya block T katika kata ya Iyela jijini Mbeya wameiomba Serikali kuwasaidia katika suala la ulinzi na kuwa makini kuwasikiliza wananchi hasa wanapopigiwa simu za hatari na wananchi.

Wakizungumza na mwanshi wetu wamesema kutokana na matukio mbalimbali yanayotokea mara kwa mara mtaani hapo na pindi wanapowataarifu kituoni wafike haraka ili kuwanusuru vibaka au wezi wanaokamatwa kwani wamekuwa wakiumizwa au kuuawa na wananchi wenye hasira kali badala ya kuwapeleka kituoni ambapo wanaweza kuwataja waharifu wenzao.

Aidha wamesema wanaomba kitendo hicho kutojirudia tena na wanaiomba serikali kuwawekea ulinzi mkali maeneo hayo kwani imekuwa kero.

Post a Comment

 
Top