Menu
 

Wakulima wa wilaya ya Kyela mkoani Mbeya wameshauriwa kusindika mazao kwa ajili ya matumizi ya baadae.

Afisa maendeleo ya jamii Bi.Nelusigwe Mwakigonja amesema ni vema wakulima wapate elimu ya kuhifadhi mazao kwa kusindika ili wanufaike na kilimo.

Pia amewashauri wakulima watembelee  maonesho ya kilimo ya nanenane katika viwanja vya John Mwakangale jijini Mbeya ili wapate  elimu hiyo.

WAISLAMU WALALAMIKIA UPANDISHWAJI WA NBEI ZA VYAKULA MKOANI MBEYA
Waisilamu jijini Mbeya wamelalamikia baadhi ya wafanyabiashara ambao wamepandisha bei za vyakula hasa katika kipindi hiki cha mwezi mtukufu  wa Ramadhani.

Bwana Omary Suleiman amesema bei za vyakula vingi vimepanda vikiwemo viazi mvilingo kutoka bei ya shilingi elfu nne kwa debe hadi elfu nne na miatano wakati gunia likiuzwa kwa shillingi elfu ishirini na saba kutoka elfu ishirini na tano vikifuatiwa na mchele,ndizi pamoja na maharage.

Kwa upande wao wafanyabiashara wamedai bei zimepanda kutokana na gharama za maisha  kupanda hivyo hata wao kujumua bidhaa kwa bei ya juu.

Post a Comment

 
Top