Menu
 


 Wamiliki wa vituo vya mafuta jijini Mbeya wamegoma kushusha bei ya mafuta iliyapangwa na kutangazwa jana na mamlaka ya udhibiti wa nishati na maji (EWURA.


Uchunguzi uliofanywa katika vituo kadhaa vya mafuta jijini Mbeya umebaini kuwepo kwa mgomo baridi ambapo baadhi ya vituo vimekuwa vikifungwa kwa kisingizio cha kutokuwa na mafuta.


Aidha uchunguzi huo umebaini kuwa katika maeneo mengine vituo vimekuwa vikiendelea kutoa huduma kwa bei ya zamani.Hapo jana Serikali ilitangaza kushasha bei ya mafuta ili kuwapunguzia makali watumiaji wa badhaa hiyo nchini.Akizungumza na wanahabari Mkurugenzi wa EWURA bwana HARUNA MASEBU amesema mafuta ya petrol yamepungua kwa shilingi 202 pointi 37 sawa na asilimia 9 nukta 17 ambapo mafuta ya dizeli yatakuwa yamepugua kwa shilingi 173 ambayo ni sawa na asilimia 8Bwana Masebu alisema alisema bei ya mafuta ya taa imeshuka kwa shilingi 181 nukta 37 sawa na asilimia 8 nukta 70 na mabadiliko hayo yametokana na marekebisho ya yaliyofanywa na kanuni kukokotolea bei za mafuta.hata hivyo baadhi ya wamiliki wa mafuta mkoani Mbeya wamekuwa wakiuza Petrol 2110 shilingi Dizeli 2015 shilingi na Mafuta ya taa Shilingi 2010.

Post a Comment

 
Top