Menu
 


Baadhi ya wananchi waishio kata ya Iyela mtaa wa Pambogo jijini Mbeya wamesema kufungwa kwa chuo kikuu cha Teofilo kisanji kumepunguza bughudha na wasiwasi wa kuvunjika kwa ndoa zao.

Wananchi hao wamesema kuwa licha ya manufaa ya kuwepo karibu kwa chuo kikuu katika maeneo yao pia wamekuwa wakikabiriwa na adha kubwa ya waume ama wake zao kuingia kwenye mahusiano ya kimapenzi kwa zaidi ya mtu mmoja.

Nao baadhi ya wafanyabishara wadogo wadogo wamesema kuwa kungwa kwa chuo hicho kumechangia kwa kiasi kikubwa kusua sua kwa shughuli zao

Mmoja wa wafanyabiashara hao Bwana Thomas Mwakalinga amesema kuwa tangu chuo hicho kilipofungwa bidhaa zao zimekuwa hazinunuliwi ukilinganisha na kipindi cha wanafunzi hao wawapo masomoni.

Post a Comment

 
Top