Menu
 

Wananchi mkoani Mbeya wameshauriwa kuzijua alama za noti mpya ili kuweza kuzitambua noti bandia kutokana na kuwepo kwa matukio ya kupewa fedha bandia hasa kwa madereva bodaboda.

Akizungumza na wananchi mkoani Mbeya Karani wa Benki kuu Bi.Zena Mapunda amesema uwepo wa fedha bandia umeongezeka hivyo kuna ulazima wa wananchi kuzijua alama za noti mpya.

Hata hivyo karani huyo amewashauri wafanyabiashara na wakulima waweze kutumia tochi za urujuani zenye uwezo wa kutofautisha noti bandia na noti halali.

Wakati huo huo Benki ya NMB Mbeya imeanzisha huduma ya pesa fasta ambayo inamuwezesha mteja kuchukua fedha popote bila kuwa na kadi ya ATM wala Akaunti.

Benki hiyo imezindua huduma hiyo mapema mwezi huu katika maonyesho ya kilimo ya nanenane mkoani Mbeya ili kuwasaidia wateja kupata fedha haraka.

Meneja wa benki hiyo Bi.Lucrensia Makiliye amesema huduma hiyo ni rahisi na ina faida kwa wananchi kupata huduma za kifedha.

Post a Comment

 
Top