Menu
 

Wananchi wa kata ya Malenga Makali mkoani Iringa wapo hatarani kukumbwa na tatizo la njaa kutokana na ukame ulioikumba kata hiyo.

Akizungumza kwenye maonesho ya kilimo ya nanenane mkoani Mbeya mtaalamu wa kilimo mkoa humo, Bwana Devi Chilagane amesema kutokana na ukame ulioikumba kata hiyo umesababisha mazao kukauka na hivyo kukosa mavuno kwa msimu mzima.

Mtaalamu huyo ameongeza kuwa mavuno kidogo yaliyopatikana yametokana na kilmo cha umwagiliaji kilichofanyika kwenye maeneo yaliyo karibu na maji.

Post a Comment

 
Top