Menu
 

Sehemu ya rangi ya Kijani ndipo ilipo Wilaya ya Mbarali
Wakazi wa kata ya Chimala wilaya ya Mbarali mkoani Mbeya wamemtaka mkurugenzi wa halmashauri hiyo kumwondoa afisa mtendaji wa kijiji cha Muela kwa muda wa siku 7 na asipotekeleza hilo watatumia nguvu ya umma kumwondoa.

Wameyasema hayo wakati wakichangia mada katika kipindi cha amka na bomba kinachorushwa hewani siku za juma tatu hadi jumamosi kupitia Bomba FM redio iliyopo mkoani humo..

Wakiongelea msimamo wao dhidi ya afisa mtendaji wa kijiji hicho Chita Chita awali wananchi wa kijiji cha Muela walikuwa wakitoa malalamiko dhidi ya uongozi wa kijiji hicho kwa kushindwa kutoa taarifa ya mapato na matumizi.

Hata hivyo baada ya tume kuundwa uchunguzi wa awali ulionesha kuwa uongozi wa kijiji ulibainika kuwa na kasoro ambapo hatua iliyochukuliwa ni wananchi kusomewa taarifa ya mapato na matumizi ambayo wamesema kuwa hawana imani nayo.

Post a Comment

 
Top