Menu
 

*Ampiga Mke wake, Mke akimbilia Kanisani.
*Mchungaji aacha Mahubiri na kuamulia Ugomvi,
*Waumini wamfikisha Mume Kituo cha Polisi Mwanjelwa afunguliwa RB na jalada.i.

Imetokea katika Kanisa la Tanzania Assemblies Of God (T.A.G) Mtaa wa Block T jijini Mbeya. Ambapo sakata hilo lilianza nyumbani pale Mme anayejulikana kwa jina la Lusekelo muumini wa Dini ya Kiislamu alipo Mkewe anayefahamika kwa jina la Bahati  avae vazi la Khanga ndipo Mwanamke huyo alivyo kaidi na kuvaa Kitenge kitendo kilicho muudhi Mmewe na kuanza kumpiga.

Baada ya kuona kichapo kikizidi Mwanamke huyo aliamua kukimbilia katika Kanisa hilo la Mchungaji Angolwisye Mwasunda akiwa Madhabahuni, hali iliyofanya ibada kuvurugika baada ya Mchungaji na waumini kuamulia ugomvi huondani ya Kanisa hilo takatifu.

Waumini walikuwa na zoezi nzito la kumdhibiti Lusekelo na hivyo kutoa taarifa Kituo kidogo cha Polisi kilichopo Mwanjelwa ambapo alifunguliwa RB hii MWNJ/RB/2630/2011. Haikuishia hapo, Mtuhumiwa aliendelea kuporomosha matusi mazito hali iliyopelekea Mkuu wa kituo cha Polisi hicho kumpeleka mtuhumiwa Lusekelo Kiruo Kikuu cha Ktai kilichopo Jijini Mbeya na kufungualia jalada/faili lenye namba MB/IR/7561/2011 kwa kosa la kufanya fujo kanisani.

Post a Comment

 
Top