Menu
 


Watu wawili wanandugu wameondolewa kwa nguvu kwenye nyumba iliyokuwa inagombaniwa kati yao na mke wa marehemu kaka yao baada ya kukaidi amri ya mahakama iliyokuwa inawataka kuondoka ndani ya siku 14

Akizungumza Dalali wa mahakama ya wilaya ya Mbeya bwana Japheti Kandonga aliwataja watu hao kuwa ni Richard Kanyasa pamoja na dada yake Neema Kanyasa ambao walikuwa wanagombania nyumba ya BI Faustina G Kanyasa mke wa marehemu Godeni Kanyasa.

Kandonga alieendelea kueleza kuwa mahakama imefikia uamuzi huo baada ya amri ya kwanza ya kuwaondoa watu hao kupingwa na mahakama ya mwanzo kitu ambacho alisema sio sahihi kisheria amri ya mahakama ya wilaya kupingwa na mahakama ya mwanzo.

Kwa upande wake bwana Richard Kanyasa alidai kuwa yeye sio mhusika wa nyumba hiyo na hivyo aligoma kuwataja watu waliopangishwa kwenye nyumba hiyo na pia alikataa kusaini kuondoka.

Post a Comment

 
Top