Menu
 

Wanawake wilayani Ileje mkoani Mbeya wameshauriwa kujiunga katika  shughuli za ujasiriamali ili kujikwamua kiuchumi hasa katika kipindi hiki cha ukombozi wa mwanamke

Akiongea mmoja wa wanawake wajasiriamali wilayani humo Bi Dinah Mtindya anayejishughulisha na ufugaji wa kuku amesema wanawake wakijishughulisha na ujasiliamali watachangia kukuza uchumi wao na wa  taifa kwa ujumla na kuondokana na janga la umasikini pia wataweza kutunza familia zao hata pindi wawapo wajane.

Naye Bi Maria John ametoa wito kwa wanawake kujenga tabia ya kuwatumia wataalamu waliopo karibu nao ili kupata ushauri  na mafunzo ya kuweza kujiendesha na kujiimarisha kiuchumi.

WAMAMU KUUNDA KATIBA MPYA MKOANI MBEYA. 
Chama cha  Jumuiya  ya waganga wa jadi Kanda za Nyanda za juu Kusini,(WAMAMU) kimekutana ili kuunda Katiba mpya itakayopelekea kutambuliwa  Serikalini.

Akizungumza wakati wa mkutano huo Katibu wa chama hicho DK.Nyalumbunde amesema Katiba hiyo itakayoundwa pia  itawasajili wanachama wake ili watambuliwe serikalini na pia imelenga kwa  wanachama wake kusaidiana pindi wapatapo matatizo kama vile kufa na kuzikana,kulipa madeni ya marehemu na kusaidia familia ya marehemu.

Akichangia hoja katika mkutano huo mmoja wa waganga hao DK. ISSA amesema uchaguzi wa viongozi wa chama chao ni vema ufanyike kila bada ya mwaka mmoja ili kurahisisha kutathmini mafanikio yaliyofanywa na uongozi uliokuwepo madarakani.


Post a Comment

 
Top