Menu
 

Wapigadebe kituoni Kabwe jijini Mbeya wameunda kikundi cha kufa na kuzikana ikiwa ni moja ya hatua ya kuimarisha umoja, upendo na mshikamano miongoni mwao.

Akiongea mwenyekiti wa umoja huo Bwana Lololo Kishoto amesema kupitia umoja huo wataweza kuwasaidiana katika shida na raha ambapo pia endapo watafikwa na msiba itawapatia urahisi wao kufanya kusimamia shughuli za mazishi.

Aidha amesema kuwa wamefungua akaunti ya umoja katika benki ya EXIM tawi la Mwanjelwa ili kuhifadhi fedha zao ambapo tatizo litakapotokea watakuwa na uwezo wa kuchukuwa fedha hizo haraka.

Post a Comment

 
Top