Menu
 

Wasichana ishirini na tisa wenye umri chini ya miaka kumi na nane wamefanyiwa upasuaji mdogo wa ugonjwa wa fistula katika hospitali ya wazazi meta mkoani Mbeya.

Akiongea nasi Mkuu wa hospitali hiyo Bi.Joyce Kasimbazi, amesema kutokana na mimba za utotoni kumesababisha wasichana hao kupata ugonjwa huo na kufanyiwa upasuaji.

Ameongeza kuwa ugonjwa huo humfanya mama kutokwa na mkojo pasipo kujizuia baada ya kujifungua, uchungu wa uzazi wa muda mrefu na kukandamizwa na kichwa cha mtoto kwenye njia ya uzazi.

Mmoja wa wanawake waliofanyiwa upasuaji huo Bi.Jane Cosmas amewataka wanawake wenzake wenye tatizo kama hilo kujitokeza katika vituo vya afya ili waweze kupata matibabu kwa kuwa fistula inatibika. 

Post a Comment

 
Top