Menu
 

Wazazi wameshauriwa kuwaeleza watoto wao faida na madhara ya uwepo wa vyuo vikuu katika maeneo yao ili kuwawezesha kijikinga dhidi ya mimba za utotoni.

Ushauri huo umetolewa na Tumaini Mwakitalu mkazi wa kata ya Iyela wakati akichangia mada juu ya faida ya uwepo wa vyuo vikuu mkoani Mbeya.

Amesema wingi wa vyuo vikuu umesaidia kwa kiasi kikubwa kuongeza kiwango cha elimu kwa wakazi wa Mbeya, Ajira na Kukua kwa uchumi.

Hata hivyo amesema licha ya faida hizo, wingi huo wa vyuo  umekuwa ukichangia migogoro ya ndoa kutokana na baadhi ya wanandoa kujiingiza kwenye mahusiano ya kimapenzi na wanafunzi wa vyuo hivyo pamoja na uongezako la Mimba za utotoni.

Aidha amewashauri wazazi kukaa na watoto wao na kuwaeleza namna wanavyoweza kujilinda dhidi ya vishawishi vinavyotolewa na wanafunzi wa vyuo vikuu hivyo.

Post a Comment

 
Top