Menu
 

Waziri wa Maji, Profesa Mark Mwandosya amesema anaendelea vizuri baada ya kufanyiwa operesheni kubwa ya mgongo nchini India.

Profesa Mwandosya amesema hayo alipozungumza kwa njia ya simu na mwandishi wetu kutoka Hospitali ya Apollo nchini India.

Amesema madaktari walimfanyia operesheni kubwa ya mgongo na kumshauri kuendelea kupata matibabu hadi afya itakapokuwa nzuri ndiyo maana hadi sasa yupo hospitali.

Mwandosya ambaye aliondoka nchini takribani miezi miwili iliyopita, amesema baada ya operesheni hiyo kwa sasa madaktari wanamfanyisha mazoezi na wamemshauri aendelee kubaki kwa muda.

Post a Comment

 
Top