Menu
 Hivi ndivyo hali ilivyokuwa kwenye kituo cha Mafuta cha GBP pale sinza Mapambano kutokana na vituo vingine vya mafuta kutofanya biashara hiyo kwa kugomea punguzo la bei lililopangwa na Serikali hivi karibuni.Kituo hiki ndicho kituo pekee kilichokuwa kikiuza mafuta kwa leo baada ya vituo kama vya BigBon TSN kuishiwa mafuta kutokana na uwingi wa watu wanaohitaji matuta kwa matumizi mbalimbali.hali hii imepelekea msongamano mkubwa wa magari katika barabara ya sinza mpaka kufikia kufungana na kushindwa kutembea kwa magari kutoka sehemu moja kwenda nyingine.Ni siku chache tu zimepita tangia Serikali itangaze kuwa imekaa na wauzaji wa mafuta na kusema imemalizana nayo na hakutakuwa na mgomo tena,lakini cha ajabu tangu siku ile hadi hii leo bado mambo ni magumu kama hivi inavyoonekana hapa.sasa sijui kunani huko chini ya kapeti??
Habari kwa hisani ya Mtaa kwa mtaa Blog

Post a Comment

 
Top