Menu
 

Mke wa Rais wa Seikali ya Mapinduzi Zanzibar,Mama Mwanamwema Shein (katikati ) akiagana na mke wa rais wa Burundi Dkt. Denise Bucumi Nkurunziza (kushoto) katika uwanja wa ndege wa Zanzibar mara baada ya kumaliza ziara yake ya siku moja visiwani humo.
Mke wa Rais wa Burundi Dkt.Denise Bucumi Nkurunziza akipatiwa maelezo ya kanisa la kihistoria na Bw. Christopher Faraji wakati alipoembelea kanisa la Anglikana mkunazini Unguja.
Mke wa Rais wa Burundi Dkt. Denise Bucumi Nkurunziza pamoja na guider wa kanisa la kihistoria la Mkunazini Ungunja Chrisopher Faraji (Mwenye shati la kitenge) wakitoka katika chemba baada ya kuangalia sehemu hiyo.
Mke wa Rais wa Burundi Dkt.Denise Bucumi Nkurunziza na ujumbe wake wakitembezwa na guider Chrisopher Faraji maeneo mbalimbali ya kanisa la kihistoria la Anglikana mjini Unguja.
Muhifadhi wa makumbusho ya Kasri Forodhani Unguja Kei Mohamed (kulia) akimpatia maelezo na kumuonyesha Mke wa Rais wa Burundi Dkt.Denise Bucumi Nkurunziza kuhusu asili ya historia ya Zanzibar na asili ya matumizi ya vitu mbalimbali alipo tembelea mahala hapo Jumba la Makumbusho ya Kasri Forodhani Unguja. (Picha na Mwanakombo Jumaa-MAELEZO)

Post a Comment

 
Top