Menu
 

 Na mwandishi wetu.
Mlinzi wa kampuni ya Leritea amehukumiwa kifungo cha miaka 30 jela kwa kosa la wizi wa magunia 84 ya zao la kokoa yenye thamani ya shilingi milioni 15, mali ya Interpres Company Litimed.

Akiongea na mwandishi wa habari hii Hakimu Mfawidhi wa mahakama ya wilaya ya Kyela Bwana Joseph Luambano amesema mtuhumiwa Bwana Piulent Mwamlewa ni mlinzi wa kampuni ya Leritea ambaye alikuwa na wenzake watatu waliochiwa huru baada ya uchunguzi wa mahakama kukamilika na kuonekana hawana hatia.

Aidha amesema kuwa mbinu iliyotumika na mshitakiwa ni kumpiga nondo mlinzi wa kampuni ya Interpres Company Limited(ICL) Bwana Lupakisyo Emanuel na kisha kuchukua mali hizo.

Post a Comment

 
Top