Menu
 

Kushoto ni Meneja Uhusiano wa Airtel Tanzania Jackson Mmbando.
++++ 
Na mwandishi wetu.
Wakazi wa kijiji cha Ibililo wilayani Rungwe mkoani Mbeya wameanza kunufaika na huduma ya mawasiliano baada ya kampuni ya simu za mkononi ya Airtel kuwasha mitambo yake kijijini humo.

Mwenyekiti wa kijiji cha Ibililo Bwana Jackson Kapoloso amesema kuwashwa kwa mitambo hiyo kutawawezesha wakazi wa kijiji hicho kuendana na mfumo wa sayansi na teknolojia katika shughuli za kijamii na uchumi.

Naye Meneja uhusiano wa kampuni hiyo Bwana Jackson Mmbando amesema uamuzi wa kampuni hiyo kuwasha mitambo maeneo ya vijijini umelenga kusogeza mawasiliano kwa jamii yote ambapo kwa mkoa wa Mbeya mitambo mingine itawashwa katika maeneo ya Ileje, Chunya, Tukuyu, Mwakaleli, Songwe, Tunduma, Uyole na Mbalizi.
 

Post a Comment

 
Top