Menu
 

  Ajali hii imetokea Majira ya Saa 2 na dakika 45 usiku, wakati dereva wa gari hilo aina ya Lori kwa lugha nyingine Tipa au gari la kubebea Mchanga akijaribu kumkwepa Mwendesha baiskeli na kulivaa gari kubwa la Mizigo lilokuwa limepaki jirani na Kituo cha mafuta cha ORXY mtaa wa Mama John Jijini Mbeya..
 Jitihada ya kuzipata namba za usajili wa ghari hilo ziligonga mwamba  baada ya kutolewa muda mfupi tuu toka kupata ajari.
  Aliyevalia Kofia ya drafti hapo katikati ni Mwandishi wa Habari na Mtangazaji wa Kituo cha Redio cha Bomba FM kilichopo Jijini Mbeya Bwana Iman John Mwakapoja akiwa eneo la tukio akiongea na wananchi walioshuhudia tukio hilo eneo la Mama John Jijini Mbeya.
 Wananchi wakiwa eneo la tukio wakishuhudia zoezi la uokoaji wa majeruhi zaidi ya watatu wa ajari hiyo ambao wamejeruhiwa vibaya lakini sikufanikiwa kupata picha ambayo inaonesha vizuri kutokana na giza. 
Tabia ya kutoa namba kwa Wamiliki wa Magari mkoani Mbeya yaendelea kwa sababu ambazo hazieleweki je?, ni kuficha ushahidi. Mpaka dakika ya mwisho tulifanikiwa kupata jina na Anwani ya mmilikiwa gari hilo ambayo ilikuwa imeandikwa ubavuni mwa gari hilo ambaye ni:- 
 Bwana Issa John.
 S.L.P 3500 
 Mbeya. 
Tanzania.
Mwananchi mmoja anusurika kufa baada ya kubata kipigo kutoka kwa Wananchi kwa kosa la kutaka kuiba taa za gari, Jeshi la Polisi la wahi kumwokoa. 

Post a Comment

 
Top