Menu
 

 Mpunga ukiwa unajazwa katika viloba.
 Mpunga ukiwa umejazwa katika viloba na mwingine ukiwa umeanikwa ili kupata fursa ya kukauka.

Na mwandishi wetu.
Bei ya mpunga na vitunguu katika soko la Sido Mwanjelwa jijini Mbeya imepanda kwa kasi hivi karibuni klwa sababu ya uchache wa bidhaa hizo(mazao).

Akizungumza na mwandishi wa habari hizi Katibu wa soko hilo Bwana Alanus Ngongwe amesema bei ya mpunga  kutoka shilingi 6,000/= hadi 10,000/= na vitunguu kwa gunia ni shilingi 55,000/= hadi 57,000/=

Aidha mmoja wa wafanyabiashara hao Bi Angela Edwini ameongeza kuwa bidhaa za vitunguu hupanda hadi kufikia shilingi 90,000/= kwa gunia moja kipindi cha masika.

Hata hivyo wafanyabiashara wameiomba serikali na halmashauri husika ndani ya jiji iwapangie bei ya moja kwa moja ilikuwaondolea kero kwa wanunuzi.

Post a Comment

 
Top