Menu
 

Na Mwandishi wetu.
Bidhaa mbalimbali za chakula zimekuwa zikipatikana kwa urahisi katika soko kuu la Manispaa ya Iringa baada ya msimu wa mavuno kuwadia.

Afisa mtendaji wa kata ya Kitanzini Bwana Frank Elias amesema kuwa upatikanaji wa mazao mbalimbali ya nafaka sokoni hapo unatokana na jitihada za Serikali na wakulima katika kutekeleza sera ya Kilimo Kwanza.

Amesema bidhaa mbalimbali kama mahindi, maharagwe, mchele, uwele na mbogamboga zimekuwa zikipatika kwa gharama nafuu ukilinganisha na awali.

Pamoja na hayo Bwana Elias ameiomba Halmashauri ya manispaa ya Iringa kuongeza ukubwa wa soko hilo ili kutoa fursa kwa wakulima wengi kutumia soko hilo kuuza bidhaa zao.

Post a Comment

 
Top