Menu
 

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
KUZAMA KWA MELI YA SPICE ISLANDERS

Usiku wa kuamkia leo Tarehe 10/09/2011 majira ya saa 9 za usiku kumetokea ajali ya kuzama kwa meli ya MV.SPICE ISLANDERS katika bahari ya eneo la Nungwi Mkoa wa Kaskazini Unguja.

Taarifa ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais,Mohamed Aboud Mohamed, imesema Meli hiyo ilikuwa ikitokea Unguja kuelekea Wete Mkoa wa Kaskazini Pemba ambapo Meli hiyo ilikuwa imepakia mizigo na abiria.

Waziri Aboud amesema Serikali inaendelea na juhudi za kukitafuta chombo hicho pamoja na watu waliokuwemo.
Amesema kwamba Serikali tayari imeshatuma vyombo vya uokozi, ulinzi na usalama katika eneo la tukio na mtakuwa mkipewa taarifa mara kwa mara.

Waziri Aboud amewataka Wananchi kuwa watulivu katika kipindi hiki kigumu na tuendelee kusikiliza taarifa za Serikali kupitia vyombo vya habari ili kupata taarifa zaidi.

IMETOLEWA NA:-
IDARA YA HABARI(MAELEZO) ZANZIBAR
10/09/2011

Post a Comment

 
Top