Menu
 


Na mwandishi wetu.
Kampeni ya kugombea nafasi ya Udiwani kwa kata za Majengo na Nzovwe zimezinduliwa rasmi katika kata ya Nzovwe kwenye viwanja vitatu tofauti.

Chama Cha Mapinduzi chenyewe kimezindua kampeni katika viwanja vya Nzovwe, CHADEMA katika viwanja vya Ndanyela wakati Chama cha wananchi (CUF) kimezindua kampeni katika viwanja vya Kilima hewa.

Katika uzinduzi huo CUF imemnadi mgombea wake Bi Dora Kambi Omary, APPT-MAENDELEO imemnadi Mwambene Fredy Mwanjo Mwambonjo, CHADEMA imemnadi David Mwashilindi na Chama Cha Mapinduzi kimemnadi Isaac Sintufya.

Afisa mtendaji wa kata ya Nzovwe Bi Joyce Weba amesema kuwa zoezi la urudishwaji wa Fomu lilifanyika katika hali ya usalama na kwamba hakuna mgombea aliyewekewa vipingamizi.

Post a Comment

 
Top