Menu
 

Katibu  wa CCM wilaya ya Mbeya Vijijini Nicolaus Kasendamila aliyeazimiwa mwanzoni mwa wiki na Jumuiya ya Vijana wa CCM wilayani humo na Baraza kuu la Wazazi kukitaka chama hicho kimuondoe hatimaye imetimia na sasa ameondolewa..
 
 Habari za uhakika kutoka wilayani humo zimeeleza kuwa katibu huyo ameondolewa na kupelekwa kusikojulikana ambapo nafasi yake imechukuliwa na Katibu wa CCM aliyekuwa wilayani Rungwe mkoani Mbeya Daud Yilanga anayetarajia kuripoti Mbeya Vijijini Jumatatu ya Septemba 5 mwaka huu.

Wakati huo huo, taarifa kutoka wilayani Rungwe mkoani hapa zimeeleza kuwa Chama hicho kimeshinda uchaguzi wa nafasi ya Mwenyekiti wa Halmashauri ya Rungwe kwa kuwabwaga wapinzani katika uchaguzi huo mdogo kwa ajili ya kuziba pengo liloachwa wazi na aliyekuwa mwenyekiti wa halmashauri hiyo aliyeuwawa mwanzoni mwa mwaka huu kwa kupigwa risasi.

Meckson Mwakipunga wa CCM ameshinda kwa kupata kura 40 huku mgombea wa NCCR MAGEUZI Anyimike Mwakasikilali akiambulia kura 3 pekee.

Post a Comment

 
Top