Menu
 


Na mwandishi wetu.
Kaimu mganga mkuu wa mkoa wa Mbeya Dakta Haruni Nyagori amesema kuwa kunauwezekano mkubwa wa mtu kupatwa na magonjwa ya ngozi endapo atashirikiana na mtu mwenye magonjwa hayo kuvaa kofia mbalimbali.

Akiongea na mwandishi wetu ofisini kwake amesema kuwa tangu kuanza kwa huduma za usafirishaji wa pikipiki maarufu kama boda boda idadi ya watu wanapatwa na magonjwa ya ngozi imekuwa ikiongezeka.

Naye kamanda wa usalama barabarani mkoa wa Mbeya Ezekiel Mgheni amesema kuwa ili kuondokana na hatari hiyo ya kupatwa na magonjwa ya ngozi madereva wa pikipiki wanatakiwa kuwavalisha Rambo wateja wao kabla ya kuwavisha kofia ili kuwakinga na magonjwa hayo.

Post a Comment

 
Top