Menu
 

Picha na Fredy Herbet (Dj Fredy) 
Moto ulianza pale majira ya asubuhi  Saa 3:50, lakini mpaka kufikia saa 5:15 Zimamoto walikuwa bado hawajafika na walipofika wakaaza kuzima moto ulikoanzia badala ya kule uelekeapo ili kunusuru mali nyingine zisiteketee.
 Na baadhi ya wafanyabiashara wamefanikiwa kuokoa bidhaa zao lakn waliowengi wamepata hasarA
Soko la Sido Mwanjelwa Jijini Mbeya ambapo chanzo cha Moto hiyo ni hitilafu ya umeme.
 Mto unaendelea kuteketeza bidhaa
Moto mkubwa ukiendelea kuwaka
 Masalia ya Bati zilizoteketezwa na Moto katika Soko la Sido.
Hili nalo ni Zimamoto ambapo wananchi wakikinga maji kwa lengo la kusaidia kuzima maji vibanda vyao. Kulia mwenye Top ya dhambarau ni AMAN MBILO Mwandishi wa habari na Mtangazaji  wa kituo cha redio cha Bomba FM kilichopo jijini Mbeya.
 Askari wa Jeshi la Kujenga Taifa JKT akiwa amemkamata mualifu ambaye alikuwa akijaribu kuiba bidhaa sokoni Hapo.
 Askari wa JKT wakimuadhibu mualifu au Kibaka
 Askari wa JKT na Polisi wakiwa wameweka chini ya Ulinzi kibaka.
Wezi na vibaka wafurahia tukio wakiwemo akina mama hili kwani imekuwa fursa kwao kutokana na kujinufaisha kwa kuiba ikumbukwe katika ajali iliyopita ya Soko la Mwanjelwa watu weki walipata mitaji kutokana na kuiba mali.

Moto ukiendelea kuchoma vibanda na makontena ya Biashara sokoni hapo.


Vyombo vya dola watumia Mabomu ya mchozi kutawanya wananchi, kwani ilikuwa haifahamiki ni nani muokoaji, kibaka na wezi baada ya kutokea kwa vurugu kubwa kwa kuwarushia mawe vyombo vya dola mara baada ya Mbunge Joseph Mbilinyi kuondoka.

Chanzo cha ajali hii ni hitilafu ya umeme na hivyo Serikali inapaswa kuimarisha kikosi cha nzima moto tukio hili ni la tatu mkoani Mbeya baada ya kuungua kwa soko la Mwanjelwa, Uhindini nah ii leo ni Sido Mwanjelwa.

Kwa mujibu wa mama moja alisikika akili milioni mbili mimi nitazitoa wapi na ndio naingia katika janga la umaskini jamani.
MMOJA WA WAFANYA BIASHARA BWANA  GODEN MWAKALINGA ALIELEZA KUWA CHANZO CHA MOTO HUO KILITOKANA NA HITILAFU YA UMEME KATIKA KIBANDA CHA BIASHARA CHA BWANA GHALIFA  NA KUSABABISHA MOTO HUO KUWAKA NA KUSABABISHA HASARA KUBWA KATIKA SOKO HILO KUU LA SIDO MWANJELWA MBEYA

Post a Comment

Anonymous said... 16 September 2011 at 15:16

kwani hawa tanesco kazi yao nn maana kila panapowaka moto umeme sasa ufanywe mkakati likitokea tatizo kama hilo na sababu ni umeme walipe ndio watAPUNGUZA DHARAU NA MALI ZA WATU

daudi said... 16 September 2011 at 15:22

Bwana mkubwa tunashukuru sana kwa taarifa hii. Thanks

UKURASA MPYA HUU said... 16 September 2011 at 17:04

Yaani wewe acha tuu tatizo wanaenda katika Vituo vya starehe na kuwaachia watu wa Field/mazoezi ambao ndio kwanza wanatoka Chuoni ambo si wazowfu na kazi hizo.....

 
Top