Menu
 

Kufuatia tamko la EWURA la kupandisha bei ya mafuta ya Diesel na Petrol kumezua malalamiko na kero kwa watumiaji wa nishati hiyo hususani madereva wa vyombo vya usafirishaji.

Akizungumza na mwandishi wetu  dereva EMMANUEL  JUMANNE amesema kupanda ghafla kwa bei za mafuta imekuwa kero  kwao, kutoka bei ya awali shilingi 2,137 hadi kufikia shilingi 2,209 kwa lita moja ya Petrol huku Diesel ikipanda kutoka shilingi 2,060 hadi kufikia shilingi 2,106 kwa lita moja.

Aidha amesema bei hizo zilitangazwa na EWURA jana hazina manufaa kwao, ukilinganisha na bei za nauli zilizopangwa na SUMATRA ambazo ni shilingi mia tatu kutoka kituo hadi kituo huku kwa maeneo ya mbali yakipangiwa kuwa shilingi mia tatu hamsini hadi mia nne.

Hata hivyo mamlaka ya udhibiti wa nishati na madini EWURA imekwisha tangaza kuwa bei ya mafuta itaendelea kubadilika kulingana kushuka na kupanda kwa soko la dunia.

Post a Comment

 
Top