Menu
 

  Gari lenye namba STK 5960 mali ya Idara ya Sheria lilokuwa likiendeshwa na Bwana Robert liligongana na Gari ya abiria lenye jina la Shapa Bup na namba ya T 999 ABP iliyokuwa ikiendeshwa na Bwana Khalifa Mussa umri wa miaka 33, mkazi wa Kabwe jijini Mbeya. Na ukawa mchezo kama wa kuigiza pale kila dereva alivyoanza kumtuhumu mwenzie kuwa ni mzembe na kasababisha ajali hiyo.
 Mtandao umebaini kuwa chanzo hicho ni Mwendokasi na hivyo Kamanda wa Polisi mkoani Mbeya Advocate Nyombi amewaonya madereva wanaosafiri kwa mwendokasi na kwamba atakayebainika hatua kali za kisheria zitachukuliwa.

Wakati huo huo Kamanda Nyombi amesema katika shughuli za Minada mizigo apakiwe kwenye maroli na abilia wapande kwenye basi kwa sababu sehemu zote barabara zinapitika kiurahisi na kwamba Amewapa wiki mbili wahalifu wa upigaji nondo ambalo linatishia maisha mkoani hapa kuacha tabia zao mara moja na dawa yao inapikwa na  Jeshi la polisi ambalo limejipanga kutokomeza tabia hizo.

Post a Comment

 
Top