Menu
 

 Mkuu wa Gereza la Ruanda Mbeya ACP Mbunda akipokea misaada ya Katoni za sabuni na Mafuta ya kupakaa
 Dr Mary Mwanjelwa akiwakabidhi Maafisa wa gereza la Ruanda.
Dr Mwanjelwa akiwa na Maafisa mbalimbali wa Gereza la Ruanda nje ya bwalo la Maafisa hao.
Na mwandishi wetu.
Mbunge wa viti maalum wanawake kupitia tiketi ya Chama Cha Mapinduzi(CCM) mkoa wa Mbeay Dk Mary Mwanjelwa ametembelea wafungwa katika gereza la Ruanda lililopo jijini Mbeya katika mfululizo wa ziara zake mkoani hapa.

Mheshimiwa Mwanjelwa katika ziara yake kwenye gereza hilo alitembelea maeneo mbalimbali kama vile sehemu za jiko, malazi pia zahanati ndogo ya gereza hilo ambapo mkuu wa gereza hilo ACP Mbunda alimtembeza maeneo hayo na baadae kuongea na na wafungwa hao na kushirikiana chakula katika gereza hilo.

Wakieleza baadhi ya kero gerezana hapo Mkuu wa gereza ACP  Mbunda alisema baadhi ya wafungwa wamefungwa kwa makosa mbalimbali ambayo mengine yangeweza kuzungumzika mtaani na wengine kushindwa kupata nakala za hukumu.tangu mwaka 1996 hali ambayo hali inayopelekea mrundikano wa wafungwa katika gereza hilo.

Kwa upande wake Mbunge wa viti Maalum Dk Mwanjelwa aliwashukuru askali hao kwa moyo wa uvumilivu kwa kufanya kazi katika mazingira magumu na kuwaasa kuwa serikari inayatambua matatizo yao na kwamba inawafanyia kazi hivyo wasife moyo kwa serikali inawajali watumishi wake.

Aidha Dk Mwanjelwa aliwaahidi kuwa kero zao itazifikisha sehemu husika na alikubaliombi lao la kupatiwa kungiamuzi cha runinga ambacho waliomba katika risala yao iliyosomwa kwake na mmoja wa wafungwa gerezani hapo.

Akihitimisha ziara yake katika gereza hilo Mbunge huyo wa viti maalum mkoani Mbeya alitoa zawadi mbalimbali kwa wafungwa hao yakiwemo mafuta ya kupakaa na sabuni za kufualia ambapo mbunge huyo alisema waupokee kwa moyo msaada huo kama ishara ya upendo kwao kwani magereza suio mahali pa adhabu bali ni mahali pa kurekebisha  mtu tabia ingawa wengine wamefikishwa hapo kwa kuonewa.

Kwa ushirikiano wa Kamanga na MatukioMbeya Yetu na Chimbuko Letu.

Post a Comment

 
Top