Menu
 

 Mtoto VANESA AMBA mwenye umri wa miaka 13, ambaye ni mwanafunzi wa shule ya msingi Ivumbwe wilaya ya Mbeya vijijini ameng'atwa na Mbwa mkono wa kuume/kulia na hivyo kupelekea kukosa msaada wa kupewa matibabu kwa kile kilichodaiwa kuwa alitakiwa kulipa shilingi 10,000/= mara baada ya kufika katika Hospitali ya Mkoa wa Mbeya
Leo hii Septemba 7 mtoto huyo anatakiwa kuanza Mitihani ya kuhitimu elimu ya Shule ya msingi, Na mpaka habari hii inaingia mtandaoni alikuwa hajapatiwa msaada wowote. Mtoto huyu analelewa na Bibi yake Bi GRENDINA FUNGO mwenye umri wa miaka 65 ambaye hajiwezi na hivyo kuomba msaada kwa wasamalia wema kuweza kunusuru maisha yake. 

Kwa habari zaidi tembelea hapa Kamanga na Matukio. 

Post a Comment

 
Top