Menu
 

  Mtoto Mpeli Mathias pichani aliyekuwa akiishi na utumbo wake nje ya tumbo baada ya kuzaliwa bila sehemu ya haja kubwa amefariki dunia mkoani Mbeya.
Mama Mzazi wa Marehemu Mpeli (Memory) Mathias, Mpeli Mwakyusa akiwa amembeba mwanae wakati wa uhai wake akiwa katika Hospitali ya Taifa Muhumbili hivi karibuni.

Taarifa kutoka kwa Mama mzazi wa mtoto huyo Mpeli Mwakyusa (26) amesema mwanae huyo alifariki dunia akiwa wilayani Rungwe mkoani Mbeya na mazishi kufanyika wilayani humo juzi.

''Mtoto ametutoka Memory wangu, Mungu awasaidie kwa msaada wenu mwendelee kwa wengine kuwasaidia, asante'' alisema Mama mzazi wa mtoto huyo kwa njia ya ujumbe mfupi wa maandishi alipowasiliana na mmiliki wa mtandao huu ambaye pia ni Mkurugenzi wa Shirika lisilokuwa la kiserikali la Tanzania Community Media Organization (TACOMO) linalojishughulisha na masuala ya kijamii.

Amesema anawashukuru wale wote waliomsaidia kipindi cha uhai wa mtoto wake ili kuokoa maisha yake lakini Mungu ndiye mwamuzi.

Mtoto huyo aliweza kupata matibabu katika Hospitali ya Rufaa ya Mbeya, Peramio na Hospitali ya Taifa ya Muhimbili baada ya kupata michango kutoka kwa wasamalia wema akiwemo Mbunge wa Jimbo la Mbeya Mjini Joseph Mbilinyi.

Taarifa ambazo zimeufikia mtandao huu wa www.kalulunga.blogspot.com ni kwamba mtoto huyo alizaliwa bila utumbo mpana hivyo alikuwa akiishi kwa majaliwa ya Mungu.

Mtandao huu unaungana na watanzania wote kutoa pole kwa ndugu jamaa na familia ya Marehemu, Mungu alitoa na sasa ametwa jina lake Lihimidiwe.

Post a Comment

 
Top