Menu
 

Mtoto huyu anaitwa Mussa Issa ni mwanafunzi wa Shule ya msingi Mbagala jijini Dra Es Salaam ambaye yupo darasa la nne, amefika jijini Mbeya akiwa hajui la kufanya na taratibu zinafanyika ili kumrejesha. Ambaye kwa kutumia basi la Sumry kwa msaada ambapo amedai alikuwa na nia ya Mkoa wa Mbeya

Mwalimu wake wa darasa anaitwa Mwalimu Athumani. Baba yake anaitwa Issa Mussa na Mama yake anaitwa Teddy Salum wote wakazi wa Gongolamboto relini.

Lakini mtoto huyu ameonekana akishinda Stendi kuu ya Mabasi yaendayo mikoa mingine ambapo watoto wengi wamekuwa wakikumbwa na balaa la Kulawitiwa kwa watoto wa kiume na watoto wa kike kubakwa.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Mtaa wa Sisimba Bi Anna Moris pamoja na Mwenyekiti wa Stendi kuu Mbeya Bwana Noah Mwakatumbula wametoa wito kwa wazazi kuwa makini na watoto hao, ambapo imekuwa kero kutokana na watoto wengi kupotea.

Post a Comment

 
Top