Menu
 

Na mwandishi wetu.
Dereva wa pikipiki Mesco Yaklini Kidope mwenye umri wa miaka 27 mkazi wa Sogea wilayani Mbozi mkoani Mbeya amejeruhiwa kwa kuchomwa kisu chini ya taya.

Tukio hilo limetokea maeneo ya sogea ambapo imeelezwa kuwa dereva huyo alikodishwa na mtu asiyefahamika ambaye wakati wakiwa safarini abiria alimuamuru dereva wa pikipiki kusimama baada ya muda mfupi abiria huyo alianza kumshambulia dereva huyo na kisha kumchoma kwa kisu chini ya taya na kumsababishia maumivu makali.

Kamanda wa polisi jijini Mbeya Advocate Nyombi amesema kuwa kijana huyo mwenye pikipiki aina ya T.BETA yenye namba za usajili T.904 BLM anaendelea kupatiwa matibabu katika hospitali ya Vwawa wilaya ya mbozi.

Post a Comment

 
Top