Menu
 

 Kijana Lusekelo Mwakanje akiwa amekamatwa muda mfupi mara baada ya kufanya utapeli wa kumuuzia Jumba la Simu aina ya Nokia lililotiwa mchanga ndani kwa Pesa za Kitanzania shilingi 25, 000/= Mwandishi wa habari na Mtangazaji wa Ushindi FM Radilo iliyopo kata ya Isyesye jijini Mbeya majira ya saa 11 Jioni eneo la Stendi ya kuelekea Wilaya ya Chunya mkabala na Soko la Sido Mwanjelwa.
 Jumba la Simu maarufu kama Housing ambayo huunzwa shilingi 2,000/= likiwa limejanzwa mchanga ndani, na hivyo kuonesha Taswira kamili ya simu ya mkononi, kwani usipokuwa makini waweza kudhania ni simu iliyokamilika.  
Taswira kamili ya utapeli huo uliokithiri Jijini Mbeya baada ya kufunguliwa tukashuhudia Mchanga na kuwafanya Abiria wengi kulinzwa na wakati mwingine kutiwa hasara.

Kijana huyo ameachiwa huru na kutuonyesha Mtandao mzima wa matapeli na Makazi yao na hivyo Jeshi la Polisi mkoani Mbeya bila shaka mwatambua hili na ni kazi kwenu sasa kushirikiana nasi bega kwa bega kutokomeza janga hili.

Post a Comment

 
Top