Menu
 

Pichani juu ni Katibu wa Taifa, Uchumi na Fedha wa CCM,ambaye pia ni mratibu wa shughuli za uchaguzi mdogo jimboni hapa kwa upande wa chama, Mwigulu Nchemba akizungumza na waandishi wa habari jana asubuhi katika ofisi za makao makuu ya CCM wilayani Igunga, kuhusu tuhuma mbali mbali ambazo CHADEMA imeituhumu CCM katika kipindi hiki cha Kampeni.


Nchemba amezungumzia kuhusu kambi ya vijana 384 wa CCM waliopata mafunzo ya kuwaongezae morali wa kukitetea chama , kambi ambayo iliwekwa katika kijiji Cha Ulemo, wilayani Iramba.


Akifafanua kuhusu kambi hiyo Nchemba alisema kuwa lengo la kambi hiyo haikuwa kuwafundisha vijana hao vurugu na kutumia siraha kama ambvyo wanatuhumiwa na CHADEMA. Alisema kuwa waliwakusanya vijana wanne kutoka katika vijiji 96 vya wilaya ya Igunga kwa lengo la kuwafundisha na kuwaimarisha kukipenda chama chao na kukitetea kwa hali na mali hususani wakati huu wa uchaguzi.


Akizungumzia kuhusu Kijana aliyemwagiwa Tindikali na watu wanaosadikiwa kuwa ni wafuasi wa Chadema, Katibu huyo wa uchumi na Fedha alisema kuwa Chadema wameshindwa kukanusha kuhusika na kitendo hicho, na hiyo ndiyo sababu hakuna hata kiongozi mmoja wa chama hicho aliyekwenda hospitali ya wilaya ya Igungas alipolazwa kijana huyo kumjulia hali kabla ya kuhamishiwa hospitali ya KCMC.


Aliongeza kusema kuwa kuna tetesi kuwa wafuasi wa CHADEMA wanapanga kumdhuru yeye kwa kumwagia tindikali. Alisema kuwa amekwisha ripoti katika chama chake, na vyombo vya ulinzi na usalama.


Alimalizia kwa kuwatuhumu CHADEMA kwa kuwaleta vijana zaidi ya 800, ambao wameletwa kutoka mikoa mbali mbali, ili wafanye vurugu katika kampeni za uchaguzi. Mwigulu alisema kuwa upo uwezekano CHADEMA wameleta makundi ya kigaidi. Alitoa wito kwa vyombo vya ulinzi na usalama kuwasaka wageni wote waliofika Igunga katika kipindi hiki cha kampeni kwani wapo ambao anaowadhania kuwa sio raia wa Tanzania .Anaripoti Victor Makinda kutoka Igunga


Post a Comment

 
Top