Menu
 

 Kijana Joshua Twaha mwenye umri wa miaka 20, makazi wa Airpot kata ya Iyela jijini Mbeya amepigwa na wananchi wenye hasira kali, katika kata ya Itezi baada ya kuvunja nyumba namba IT/431 mali ya Bwana Mwansyange Pambeje mwenye umri wa miaka 45 wakati hawapo nyumbani hapo na kukumbana nae uso kwa uso mwizi akiwa na shoka na kumtishia mmiliki, ndipo mmiliki akapiga yowe kutaka msaada. 
   Mara baada ya kupekuliwa alikutwa na Vitambulisho viwili kimoja kikiwa kinaonesha kwamba ni Mwanafunzi wa shule ya Sekondari Irambo na kingine kikionesha kuwa ni Mfanyabiashara wa eneo la Mwanjelwa.
 Marabaada ya mtandao huu kuwasikiana na Jeshi la Polisi na hivyo kufanikiwa kufika mapema na kumwokoa
 Akihojiwa na Askali wa Upelelezi.
 Kijana Joshua akiongozana na askali wa upelelezi kuelekea kwenye gari.
Akiamulishwa kupanda katika gari la Jeshi la polisi.
 Mlango wa chumbani kukiwa kumevunjwa
Bwana Mwansyanje akishangaa mara baada ya tukio hilo kutokea.
  Mama huyu Bi Maria Fredy ambaye nyumba yake namba IT/439 kata ya Itezi Uyole akishngaa mara baada ya kurudi nyumbani kwake na kukuta kumevunjwa wakati akitoka kuangalia tukio la kwanza la nyumba iliyovunjwa kwa jirani yake ambapo mama huyo aliibiwa vitu kadhaa ambavyo thamani yake haikuweza kufahamika.
 Begi likiwa limechanwa na kuchukuliwa kila kiyu kilicho kuwemo humo.
  Mwanafunzi akishangaa Chumbani kwake kumevunjwa na kuibwa baadhi ya vitu vyake.

 Mtuhumiwa Joshua Twaha anashikiliwa na Jeshi la polisi Kituo cha Kati jijini Mbeya.
Picha na habari kwa ushirikiano na Mbeya YetuKamanga na Matukio na Chimbuko Letu.

 WEZI WACHACHAMAA LICHA YA KUPOKEA KIPIGO CHA KUTISHA, KUCHOMWA MOTO NA KUUWAWA.

Post a Comment

 
Top