Menu
 

 Na mwandishi wetu.
Afisa elimu mkoa wa Mbeya Bwa Juma Kaponda amesema utafiti wa awali umeonesha kuwa wanafunzi wa shule za msingi wamekuwa wakifeli mitihani yao kutokana na kusoma wakiwa na njaa hivyo kushindwa kuelewa wafundishwapo wawapo darasani.

Wakati huohuo amewataka wazazi kushiriki kikamilifu katika kutoanguvu kazi na  michango itakayowezesha ukarabati wa shule pindi madarasa yanapoharibika ili kutoa nafasi kwa wanafunzi kusoma katika mazingira mazuri.

Awali wakazi wa mji mdogo wa Mbalizi, eneo la Mlima reli walise,a watashiriki kuchangia chakula kwa wazazi wanaosoma katika shule ya Msingi Mlima reli, endapo serikali itaboresha miundombinu ya shule hiyo.

Wakiongea na mwandishi wetu wamesema itakuwa jambo la aibu kwa wanafunzi kuboreshewa chakula wakati wakisoma katika madarasa mabovu huku shule ikiwa haina huduma ya maji safi na salama. 

Post a Comment

 
Top