Menu
 


Na Mwandishi wa Jeshi la Polisi-Kagera
Polisi mkoani Kagera wamemuua kwa kumpiga risasi mmoja ya wachimba madini wadogo waliokuwa wakijaribu kumchoma moto mwenzao mmoja aitwaye Samwel Marwa (28), Mkazi wa Kijiji cha Runzewe, Wilaya ya Bukombe, Mkoani Shinyanga kwa tuhuma za kuwaibia madini yao.
Kamanda wa Polisi mkoani Kagera Henry Salewi amesema kuwa katika harakati za kumuokoa kijana huyo pia Askari Polisi wawili wamejeruhiwa kwa kushambuliwa kwa mawe na wachimbaji hao wa madini wakati walipokuwa wakimuokoa mmoja ya wachimbaji hao aliyekuwa akichomwa moto kwa tuhuma za wizi wa madini.
Kamanda wa Polisi mkoani Kagera SACP Henry Salewi, amewataja Askari waliojeruhiwa kuwa walifanikiwa kumuokoa kijana huyo, lakini Askari wawili F. 5609 D/CPL. Daniel Wangiboma na G. 3568 PC Ntimbula Bakari walijeruhiwa kwa mawe vichwani na wamekimbizwa katika Hospitali ya wilaya ya Biharamulo kwa matibabu.
Amesema siku ya tukio hilo jana Polisi wa Kituo kidogo cha Mavota kwa kushirikiana na Askari Polisi wa Operesheni Wilayani Biharamulo, walimuua mtu huyo ambaye hajafahamika jina lake wakati wakiwa katika harakati za kumuokoa kijana huyo.
Kamanda Salewi amesema kuwa, marehemu ambaye hajafahamika jila lake, alikuwa ni miongoni mwa kundi la wachimbaji waliokuwa wakimshikilia kijana huyo na kuwashambulia Polisi kwa kuwapiga kwa mawe ili kutomuokoa kijana waliodai amewaibiua madidi yao.
Kamanda Salewi amemtaja kijana aliyetunusurika kuchomwa moto kutokana na wizo huo ambaye pia bado anahojiwa na Polisi kuwa ni Samwel Marwa (28).
ambaye alikuwa amekamatwa na kundi la wachimbaji wadogo wadogo wapatao 100 kwa nia ya kumchoma moto kwa madai kwamba Samwel alikuwa amewapora dhahabu zao.
Amesema mara baada ya kuona maisha ya kijana huyo yalikuwa hatarini, baadhi ya wananchi walikimbia katika kituo kidogo cha Polisi cha Mavota Wilayani Biharamulo ambapo kwa kushirikiana na askari Polisi walioko kwenye Operation maalumu eneo la Mgodi wa Madini madini ya dhahabu wa Tulawaka unaomilikiwa na Kampuni ya Barrick, walikimbia kwenda kuokoa maisha ya kijana huyo.
Amesema kuwa walipokaribia kwenye kundi la watu hao, Polisi walianza kushambuliwa kwa mawe na kujaribu kufyatua risasi hewani bila ya mafanikio na ndipo walipompiga mmoja na kuanguka na wengine kukimbia na kufanikiwa kumuokoa kijana huyo.
Askari hao pia wamefanikiwa kupata mafuta lita tatu aina ya Petrol ambayo ilikuwa itumike kwa kumchomea moto kijana huyo.
Amesema kuwa katika tukio hilo watu wanne walikamatwa kuhusiaka na jaribio hilo la mauaji na amewataja waliokamatwa kuwa ni Jejo Motopasi(26) Simon Motopasi(22) na James Vicent(20) wote wakazi wa Kiji cha Runzewe Wilaya ya Bukombe na Vicent Idian(25), Mkazi wa Kijiji cha Mavota Wilayani Biharamulo.

Post a Comment

 
Top