Menu
 

Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Bwana John Livingstone Mwakipesile (wa kwanza kutoka kulia).

Na mwandishi wetu.
Mkuu wa mkoa wa Mbeya Bwana John Livingsone Mwakipesile ametoa wito kwa washiriki wa Mafunzo ya Utafiti wa Mapato na Matumizi ya kaya binafsi kuzingatia maadili ya kazi ikiwa ni pamoja na kutoa takwimu sahihi ili wapanga maendeleo na watoa maamuzi kutekeleza majukumu yao ipasavyo.

Ameyasema hayo kwa nafasi ya ugeni rasmi alipokaribishwa na meneja utawala wa ofisi ya Taifa Takwimu Bwana Gabriel Madembwe kwa niaba ya Mkurugenzi mkuu wa ofisi hiyo ambapo mafunzo hayo yanaendelea katika ukumbi wa Tughimbe Mbalizi .

Kwa upande wake Madembwe amesema mafunzo hayo yamejumuisha washiriki 81 kutoka mikoa ya nyanda za juu kusini na madhumuni ya utafiti huo ni kupata taarifa kutoka ngazi ya kaya zinazohusu shughuli za kiuchumi umiliki na hali ya majengo yatumikayo na kaya mapato na matumizi, viwango vya elimu, hali ya afya na mengineyo.

Aidha mafunzo hayo yamehudhuliwa na meneja wa ofisi ya Taifa ya Takwimu Mkoa wa Iringa Ruvuma Rukwa na mwenyeji wao Bi.Theresia Lymo ambaye ndiye meneja wa ofisi ya Taifa Takwimu mkoa wa Mbeya.

Post a Comment

 
Top