Menu
 


Wafanyakazi wa Kampuni ya Ulinzi maarufu kama Gema Security Tawi la Mbeya, ambalo makao makuu  yake Jiji Dar es Salaam, wakiwa nje ya Mahakama ya Kazi jijini hapa wakidai malipo yao baada ya kuachishwa kazi. Licha wakiwa wamelinda kwa uaminifu majengo yenye Mamilioni ya Bidhaa ikiwa ni Pamoja na Hospitali ya Meta, Rufaa, Ustawi wa Jamii na mengineyo.

Hawajalipwa madao yao na Mwajiri wao akidai kuwa Wizara ya Afya haijaweza kumlipa fedha za lindo, ambapo inatia shaka uwezo wa kampuni hiyo juu ya utendaji na haki za wafanyakazi wake.


"Serikali iangalie kwa umakini suala la Makampuni ya Ulinzi ili kuwawezesha walinzi kupata haki zao za msingi kutokana na kulipwa mishahara ya kima cha chini kabisa,  licha ya kufanya kazi kwa kujituma na kwa umakini na wengine kushindwa kulipa kiinuo mgogo kwa wakati muafaka mara baada ya wafanyakazi wao kustaafu".

Post a Comment

 
Top