Menu
 


Na mwandishi wetu.
Siku 3 zimesalia kufanyika kwa uchaguzi mdogo katika kata za Nzovwe na Majengo ambapo maandalizi kwa ajili ya uchaguzi huo yanaendelea vizuri.

Majina ya watu wenye sifa za kupiga kura yamebandikwa katika mbao za matangazo ofisi za maafisa watendaji wa mitaa na kata hata hivyo kumetokea malalamiko kadhaa kutoka kwa baadhi ya wananchi ambao majina yao hayajabandikwa.

Wagombea wanaowani nafasi ya Udiwani kwa kata ya Nzovwe ni OMARY AHAMED kupitia Chama Cha Wananchi (CUF), DAVID MWASHILINDI kupitia CHADEMA, SHABANI MBEGU kupitia NCCR- Mageuzi, FREDY MWAMBONDO kupitia APPT MAENDELEO na ISAAC SINTUFYA kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM)

Aidha vyama vya siasa vitafunga kampeni za kuwanadi wagombea wao octoba mosi ambapo kampeni za Chadema zitafungwa na Mbunge wa viti maalumu na mjumbe wa BAVIJA Taifa NAOMI MWAKYOMA wakati kampeni za Chama Cha mapinduzi zitafungwa na katibu mwenezi wa siasa wa CCM mkoa Emanuel Madodi.

Post a Comment

 
Top