Menu
 

Huyu ni Mbunge wa Jimbo la Ileje mkoani Mbeya kupitia CCM Bwana Nikusukuma Aliko Kibona.
Taasisi za kidini jijini Mbeya zimeshauriwa kuwasaidia watoto yatima na wanaoishi katika mazingira magumu kupata Elimu badala ya kuwaacha wakizurula mitaani.

Ushauri huo umetolewa hivi karibuni na Mbunge wa jimbo la Ileje Mheshimiwa Nikusukuma Aliko Kibona katika moja ya ibada za kanisa la Brotherhood lililopo eneo la Majengo jijini ambapo mbunge huyo amepewa nafasi ya kuongea na waumini wa dhehebu hilo.

Amesema kuwasaidia watoto wadogo kuna baraka kubwa kwa Mwenyezi Mungu, hivyo kila muumini wa Kikristo ana wajibu wa kutumia uwezo alionao kutoa msaada kwa watoto yatima na wale wanaoishi kwenye mazingira hatarishi ili kuwajengea uwezo wa kujitegemea hapo baadaye.

Post a Comment

 
Top