Menu
 


 Na mwandishi wetu.
Mamlaka ya Chakula na Dawa imewataka wafanyabiashara wa vyakula dawa vipodozi na vifaa tiba kupeleka matangazo yao katika ofisi ya mamlaka hiyo kabla ya kuyatangaza ili mamlaka ithibitishe kama hayana upotoshaji kwa watumiaji.

Akizungumza na mtandao huu Meneja wa Mamlaka hiyo Nyanda za juu Kusini Bwana Lazaro Mwambole amesema kuna baadhi ya wafanyabiashara ambao wamekuwa wakitangaza bidhaa zao mbalimbali kinyume na sheria kiasi cha kuhatarisha afya za watumiaji hasa pale bidhaa hizo zinapokosa ubora.

Aidha Mwambole amesema hapatakuwa na gharama zozote wala urasimu katika kupata kibali cha maandishi na kwamba kila tangazo lazima liombewe kibali na kibali kitatolewa baada ya tangazo kuthibitishwa na kufanyiwa marekebisho inapobidi.

Pia ametoa wito kwa jamii kutambua kuwa kulinda afya zao ni jukumu lao pamoja na serikali hivyo ni vema kwa wanajamii kuwafichua wanaokiuka taratibu za mamlaka ya chakula na dawa ili  wachukuliwe hatua.

Post a Comment

 
Top