Menu
 

Meneja wa mauzo mikoa ya Mbeya na Rukwa Kevin Mibazi (kulia) 
Na mwandishi wetu.
Kampuni ya simu za mikononi TIGO imeandaa tamasha lijulikanalo kama TIGO Sells Convention jijini MBEYA lililowakutanisha mawakala mbalimbali kutoka mikoa ya nyanda za juu kusini kwa lengo la kufahamiana na kubadilishana uzoefu wa kikazi.

Akizungumza na mwandishi wetu Meneja wa mauzo wa Tigo KELVIN MIBALI amesema tamasha hilo litakuwa likifanyika kila mwaka kwa malengo ili kuboresha utendaji kazi wa kampuni hiyo.

Tamasha hilo lililoanza kwa mchezo wa mpira wa miguu ambao uliikutanisha timu ya mawakala wa Mbeya na mawakala wa Songea ambapo timu ya Mbeya iliibuka na ushindi wa goli sita kwa tano.

Post a Comment

 
Top